Kisii: DP Ruto Atokwa na Kijasho Kuendesha Basi Aliloikabidhi Shule
Naibu Rais William Ruto, wakati wa ziara yake ya siku tatu katika kaunti ya Kisii, alitoa mabasi matatu kwa Shule za Sekondari za Bogichoncho, Nyakembene na Kiabigoria. Wakati wa sherehe ya Jumatatu, Oktoba 4 huko Mugirango Kusini, umati wa watu ambao walikuwa wamehudhuria hafla hiyo walimpa changamoto DP huku wakimtaka kuendesha mojawwapo ya mabasi hayo.